Jumatatu, 24 Oktoba 2016

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

Habari rafiki?
Nimatumaini yangu u mzima na unaendelea na shughuli za kujenga taifa
Leo napenda tuzungumzie kuhusu kufanya mazoezi,
Kuna jamaa angu huwa anamwili mdogo sana yani mwembamba nilimuuliza unafanyaje mpaka unakuwa na mwili mwembamba kiasi hiki wakati kwanza hufanyi hata mazoezi?  akasema kwanza huwa sili mchàna halafu ikitokea hata jioni sili kabsa,
Sikuwa na cha kujifunza kabsa.

Kuwa na afya bora ni msingi wa mafanikio yote.
Hata uwe  na mipango mikubwa vp kama una afya mbkvu huwezi kufanya kitu chochote.
Unapokuwa na afya bora inakupa nguvu na kuishi maisha bora wakati wote bila ya kuteteleka.

Katika mazingira yetu afya zote zinaamuliwa na vyakula
Tunavyokula .
Na maisha tunayoishi karibu kila siku ndiyo inayotuamulia afya zetu ziweje sasa na badae.
 
Kama unaishi maisha ya ulevi, uasherati na kulakula hovyo usitegemee afya bora katika maisha yako.
Vilevile kama hujihusishi na mazoezi usahau kuhusu afya bora.
Ili ufanikiwe tambua kitu cha kwanza ni afya bora .

Watu wengi tunaona mazoezi ya mwili yakifanyika lakini hatujui faida zake.
Zipo faida nyingi lakini mimi naomba nikushirikishe hizi chache

1- Mazoezi ya mwili husaidia kurekebisha shinikizo la damu
2- Huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kufanya miguu na mikono ipate joto.
3- Yanaondoa mambo yote mawili
Yani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo na kukusadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako, pia ni tiba bora kabsa ya kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo
4- Katika utaft wa kisayansi mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva.
Pia yanaongeza afya kwa kuamsha mfumo wa kinga mwilini.
Mwili upowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaaa ubongo unakuwa na uwezo wa kufikria kwa ubunifu na ufanisi mkubwa zaidi.

5-    Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili.
Pia hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi na inakuchukuwa muda sana wewe kuwa na uchovu kimwili na kimawazo .

6     Yausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kusitahimili maumivu.

       Kila la heri rafiki yangu nakutakia siku njema asante kwa kutembekea blog yangu hiii
Unaweza kunipata kwa barua pepe jilalajoseph@gmail.com au namba
0766836833 namba ya Whatsapp 0621116197 nashirikiana mambo mengi yanayohusu mafanikio katika maisha yetu asante sana na karibu tena