Ijumaa, 4 Novemba 2016
KUWA NA MAONO NA KUWEKA MALENGO. Anza Mwaka 2016 kwa kuandika Mipango Yako, ndiyo ramani kuu ya Mafanikio . Umewahi kujiuliza mtu anayetembea njiani , hapajui anakokwenda na hivyo haijui njia.Akifika njia panda akamkuta mtu , atamuuliza “ NIFUATE NJIA IPI ?” Ni lazima naye atamuuliza “ UNATAKA KWENDA WAPI ? “ Akijibu “Sijui”, uwe na uhakika yule anayetegemewa kuelekeza atajibu “ CHAGUA NJIA YOYOTE UIPENDAYO KATI HIZI NNE ITAKUFIKISHA POPOTE”. Huyu hana MAONO kwahiyo ni lazima atajikuta katika matatizo tu ! HAJITAMBUI ! Kundi hili ni kubwa sana katika jamii yetu wengi wao ni wale wasio na MAONO maishani mwao.Wanaishi tu kwa hapa na sasa.Hawana ndoto,malengo wala kitu mbeleni. Hawajatimiza NDOTO zao wala nini , bali wapo tu !! Ndio wale husherehekea MWAKA MPYA kwa fujo sana kwa kuchoma mipira, kupiga baruti , kufanya fujo , wizi n.k. bila kujiuliza MASWALI YA MSINGI. Mtu unapaswa KUJITAMBUA-----WEWE NI NANI ? UMETOKA WAPI ? UNAKWENDA WAPI ? KUFANYA NINI ? NA KWANINI ? UKO WAPI ? UNAFANYA NINI ? KWA NINI UNAISHI . Na siyo kuishi tu bora upo au bora liende ! HAPANA BADILIKA NDUGU YANGU . Katika SAFARI YA MAISHA YA MAFANIKIO, MAONO NA MALENGO vina nafasi kubwa sana katika kuwa na mwelekeo maalumu wa utendaji ,bila hivyo hutafanya lolote bali utabaki kulalamika kila mwaka unaopita na mwisho wa siku utajikuta hueleweki. Inakuwa sawa na gari bila usukani. Gari hii haiwezi kuekekea mahali kunako takiwa,itapoteza mwelekeo .Wakati MAONO yakiwa kama DEREVA mwenyewe , MALENGO kwa upande wake ni USUKANI.Hukuongoza na kukupeleka unakokutaka. Ufanye lipi miongoni mwa mengine. Bila MAONO kasha MALENGO hautafanya jambo la maana. MAONO----DEREVA MALENGO----USUKANI ANGALIZO: Bila MAONO kisha MALENGO hautafanya jambo la maana ndugu yangu. Ndugu yangu kukosa MAONO maishani ni hatari. Hata maandiko matakatifu ,imeandikwa hivi ; “Pasipo maono , watu huacha kujizuia “ Mithali 29:18a , maana yake Pasipo maono , watu hushindwa kujizuia katika mambo yasiyofaa kama ulevi , wizi , zinaa n.k. ambapo mwisho wa siku utajikuta matatizoni. watu hufanya mambo kiholela , hawana kitu cha kuwawekea mipaka , hawana chochote cha kuwasukuma kulifuatilia jambo kulitekeleza mpaka wakalifikikisha mwisho wake. Kama hauna MAONO katika maisha yako hata MAISHA yenyewe yatakuwa hayana msimamo. Kuna msemo wa Kiingereza unasema “An idle brain is the devil workshop” maana yake AKILI isiyojishughulisha ni karakana ya SHETANI. “Hakuna kitu kikubwa hapa duniani kilichofanyika bila maono na shauku”. ---Georg Wilhelm Friedrich Hegel. Watu wengi wanafeli maishani si kwa sababu ya kukosa uwezo au ubongo au hata UJASIRI bali ni kwa sababu hawajakusanya nguvu zao katika MALENGO.”----Elbert Hubbard. MAONO NI NINI ? MAONO (VISION) kwa maneno mengine tunaweza kusema NDOTO ni picha au matazamio anayokuwa nayo mtu, shirika au taasisi juu ya ufanisi katika jambo fulani. NINI TOFAUTI YA MAONO NA MALENGO ? Wakati MAONO yakiwa ni jumla ya picha ya MAFANIKIO, MALENGO kwa upande wake ni kiwango/ kiasi cha mafanikio ayatakayo mtu / taasisi ndani ya kipindi fulani. Tofauti na MAONO ambayo kwa kawaida huwa hayawekwi katika kiwango na MUDA maalumu , MALENGO huwa katika kiwango na MUDA maalum. Kwa mfano , unapanga kwamba katika kipindi fulani nataka niwe sehemu fulani katika jambo fulani.Hayo ndiyo MALENGO. KWA MFANO , MALENGO yako yanaweza kuwa--------“nataka kuwa na magari saba ya biashara ndani ya miaka mitano “. Hapo MAONO ni kuwa na magari ( bila shaka mengi tu ) ya biashara. Lakini MALENGO ni kuwa nayo saba ndani ya miaka mitano. .” NI HATARI SANA hivi ndivyo alivyo mtu ambaye anategemewa KUFANIKIWA lakini hana DIRA /MUELEKEO----yaani hana MALENGO. ANGALIZO: Kama huijui NJIA ya unapokwenda , hakikisha unayo RAMANI YA NJIA unayotakiwa kuipita , mikononi mwako. RAMANI ni dira ya safari . Inaweza kukuongoza mpaka mwisho wa safari yako kama ukifuata jinsi inavyoelekeza au jinsi ulivyoipanga WEWE MWENYEWE. MALENGO ni DIRA ya mtu.Ni dira ya huko ankotaka kufika. Ni lazima uwe na MALENGO au DIRA kabla hujaanza SAFARI YA MAFANIKIO. Kwa kawaida , MALENGO yote huwekwa mwanzoni mwa safari. Watu wasipokuwa na MAONO kisha MALENGO , hawawezi kuwa na MWELEKEO wa kiutendaji. Hawawezi kujipa NIDHAMU YA UTENDAJI maana hawana na hawajui wanapokwenda. UNAFIKIRI nini kitawasukuma kufanya BIDII ili hali hawajui umbali wanaotakiwa kusafiri kabla ya muda fulani na kwa ufanisi kiasi gani ? Na je ! Lini watajua wamefika ? Watapimaje ufanisi wenyewe ? NAMNA YA KUWEKA MALENGO Jambo linalopelekea wengi wetu kutofanikwa ni kukosa kuweka MALENGO yanayoeleweka na yanayotekelezeka kulingana na MAZINGIRA, MUDA, NYENZO , n.k. Kuna mambo ya kuangalia/ kuzingatia kabla hujaamua kuweka malengo.Unapaswa kutulia katika hili kwani hayo ndiyo MAISHA yako. Zipo dondoo kadhaa katika namna ya kuweka MALENGO ili uweze kupata ufanisi katika SAFARI YA MAFANIKIO kama ifuatavyo :-- (1).LENGA ENEO NA SHUGHULI MAALUM. Shughuli na maeneo ya kufanikiwa ni mengi mno.Mambo ni mengi .Huwezi kushughulika na kufanikiwa yote.Lenga jambo moja au mawili tu.Kama ni biashara basi jikite huko.Baadhi ya maeneo ya kufanikiwa ni kama vile Sanaa ,biashara , Michezo, Uvumbuzi katika teknolojia ya matumizi ya kompyuta na mawasiliano ya mtandao n.k. (2).WEKA MALENGO MAALUM NA YANAYOPIMIKA. Ili uweze kufanikiwa vyema, unatakiwa kuweka MALENGO yanayoeleweka , maalum na yanayopimika kiasi kwamba unaweza kwa wakati wowote kupima / kutambua umeyafikia na kiasi gani. (3).WEKA MALENGO MAKUBWA KIASI KWAMBA UKISHINDWA KUYAFIKIA BADO UWE UMEFANIKIWA: Hii inasaidia ubongo kuwaza sana na kujishughulisha kwa kiwango cha juu zaidi ambapo mara kadhaa hupelekea mafanikio. Utafiti unaonyesha kuwa kadri unavyopania / kulenga jambo kubwa ndivyo akili yako inajiweka katika KUFIKIRIA na KUTENDA kikubwa zaidi. (4).WEKA MUDA MAALUMU KATIKA MALENGO YAKO: Kumbuka kuwa MALENGO huenda na MUDA. Bila kujiwekea MUDA hautapata msukumo wa kutenda kwa WAKATI. Pasipo na MUDA hautaweza kujitathmini---kuona nini umekifanya / kukipata katika kipindi Fulani. Kuweka MALENGO YA MUDA MREFU na MALENGO YA MUDA MFUPI kama mwaka mmoja. JIPANGIE MUDA , JIBANE na JISIMAMIE WEWE MWENYEWE. SIFA ZA MALENGO MAZURI ----Lengo ni lazima liwe MAALUM na liwe linaelezeka. Mfano lengo la kuwa daktari bingwa wa watoto. ----Lengo lililowekwa vizuri siku zote huwa LINAPIMIKA. ---Lengo zuri lazima liwe LINATEKELEZEKA. ----Lengo lazima liwe LINAFIKIKA. -----Lengo zuri ni lazima liwekewe MUDA wa utekelezaji. VISION—An idea or picture in your imagination. GOAL---Something that you hope to achieve. Makala hii imeandikwa na MWL JAPHET MASATU , Mwandishi, mwelimishaji, , mhamasishaji katika masuala ya kimafanikio, ujasiriamali ,biashara na mambo ya kimaisha kwa ujumla .Anapatikana kwa namba : Call / WhatsApp +255 755 400 128 / +255 716 924 136. E-MAIL : japhetmasatu@gmail.com. 01/01/ 2016 Ijumaa. Posted by MWL . JAPHET MASATU at 4:24 AM Reactions: Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Pinterest Labels: MAISHA NA MAFANIKIO No comments: Post a Comment Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni